Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema Iran ina haki ya kutumia teknolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya amani, na Urusi iko tayari kuisaidia kama ilivyofanya hapo awali.
Akizungumza baada ya kikao cha SPIEF, Putin alieleza kuwa Urusi inapinga uenezaji wa silaha za nyuklia, na alitaja kuwa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) halijathibitisha ushahidi wowote kuwa Iran inalenga kutengeneza silaha hizo.
Kauli hii imekuja wiki moja baada ya Israel kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran ikidai kuwa taifa hilo linaelekea hatua ya hatari katika kutengeneza silaha za nyuklia – madai ambayo Tehran imekanusha vikali.