Marco Aitaka China Kuzuia Iran Kufunga Mlango

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

14 hours ago
rickmedia: marco-aitaka-china-kuzuia-iran-kufunga-mlango-786-rickmedia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ameitaka China kuizuia Iran kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, mojawapo ya njia muhimu zaidi ya meli duniani

Ametoa maoni yake baada ya televisheni ya taifa ya Iran Press TV kuripoti kuwa bunge limeidhinisha mpango wa kufunga Mlango Bahari huo lakini likaongeza kuwa uamuzi wa mwisho ni wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa.

Usumbufu wowote wa usambazaji wa mafuta unaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi. China haswa ndiyo mnunuzi mkubwa zaidi wa mafuta ya Iran duniani na ina uhusiano wa karibu na Tehran.

Bei ya mafuta ilipanda kufuatia mashambulizi ya Marekani kwenye maeneo ya nyuklia ya Iran, huku bei ya mafuta ghafi ikifikia kiwango chake cha juu zaidi katika muda wa miezi mitano.