Tovuti ya Illicit Encounters nchini Uingereza, inayowahudumia watu walio kwenye ndoa wanaotafuta mahusiano ya siri, imetoa ripoti ikionesha kuwa wauguzi wa kike ndio kundi kubwa zaidi la wanawake wanaotumia jukwaa hilo.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, sababu kuu zinazochangia hali hiyo ni kazi zenye muda mrefu, msongo wa mawazo na changamoto za kihisia zinazowakumba wauguzi. Wataalamu wa saikolojia wanasema mazingira haya ya kazi yanaweza kusababisha umbali wa kihisia kati ya wenzi, na hivyo kuongeza uwezekano wa mtu kutafuta faraja au uhusiano nje ya ndoa.
Hata hivyo, wataalam wanaonya kuwa matokeo haya hayamaanishi kila muuguzi yuko katika hatari hiyo, bali yanadhihirisha changamoto za maisha ya kazi zinazohitaji uelewa na msaada wa kijamii.