Aliyekuwa mpenzi wa marehemu rapa A.K.A ambaye yeye pia ni rapa wa kike wa Afrika Kusini Nadia Nakai amemtambulisha mpenzi wake aliyemuandika kwa jina la Ryan kupitia post ya Instagram akimtakia kheri ya siku ya kuzaliwa.
Nadia amemuandikia ujumbe mrefu wa kheri ulioambatana na maelezo ya namna anavyojisikia faraja tangu ampate mwanaume huyo kama mpenzi wake.
A.K.A alifariki February 10, 2023 akiwa na Miaka 35 kwa kupigwa risasi huko Durban, South Africa na tangu mwaka huko Nadia hajawahi kupost kitu chochote kuhusu mahusiano mapya mpaka leo hii.