Mkazi wa Kijiji cha Mungushi, Wilaya ya Hai, Mary Mushi (26), anadaiwa kuwaua watoto wake wawili, mmoja mwenye umri wa miaka minne na mwingine wa miezi sita, kisha kujaribu kujiua kwa kujijeruhi, katika tukio la kusikitisha linalodaiwa kusababishwa na mgogoro wa kifamilia.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Abel Mtagwa, amethibitisha kutokea tukio hilo mchana wa Juni 20, 2025, na kusema kuwa uchunguzi umeanza ili kubaini chanzo cha tukio hilo.