Chris Brown Akana Mashtaka Ya Kumpiga Mtu Club

-rickmedia: Rick

Rick

19 hours ago
rickmedia: chris-brown-akana-mashtaka-kumpiga-mtu-club-245-rickmedia

Staa wa Muziki #ChrisBrown amekana mashtaka ya shambulio baada ya madai ya kumshambulia mtu kwa chupa mjini London miaka miwili iliyopita.

#Brown, mwenye umri wa miaka 36, anashtakiwa kwa kujaribu kusababisha madhara ya mwilini kwa mtayarishaji wa muziki #AbrahamDiaw katika Club huko London.

Waendesha mashtaka wanadai kwamba #Diaw alipigwa mara kadhaa kwa chupa katika shambulio lisilo la kuchokozwa na baadaye kupigwa ngumi na mateke.

Mshitakiwa mwenzake #Brown, #OmololuAkinlolu, anayejulikana kwa jina la kisanii #HoodyBaby, naye pia amekana mashtaka hayo.

#Brown anakabiliwa pia na mashtaka ya kusababisha madhara ya mwilini, pamoja na kuwa na silaha hatari kama chupa ya tequila. Mashtaka yote yanahusiana na tukio hilo hilo.