Mwanamuziki #RKelly amekataliwa kuachiwa kutoka gerezani siku chache baada ya mawakili wake kudai kuwa alipewa alizidishiwa dozi ya dawa mpaka kupoteza fahamu kwa makusudi katika jaribio la mauaji lililoshindikana.
Timu yake ya wanasheria ilikuwa imewasilisha ombi la kumhamishia kwenye kifungo cha nyumbani kutokana na maisha yake kuwa hatarini Gerezani.
Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Marekani, Martha M. Pacold, aliamua kwamba ombi la Kelly liko nje ya uwezo wake katika amri iliyotolewa siku ya Alhamisi. Jaji huyo wa Chicago alibainisha kuwa ili mfungwa kutumia kesi ya haki za kiraia kupinga hali ya kifungo chake, ni lazima pia awasilishe ombi la hati ya habeas corpus.
Hata hivyo, hata kama ombi la Kelly la Juni 10 lingeweza kuchukuliwa kama ombi la habeas corpus, Pacold alisema bado asingekuwa na mamlaka ya kulitolea uamuzi kwa sababu “mamlaka ipo katika wilaya moja tu: wilaya ya kifungo. Kelly kwa sasa anahifadhiwa katika FCI Butner, ambayo iko Butner, North Carolina nje ya wilaya hii ya kimahakama. Kwa hivyo, mahakama hii haiwezi kumpa msaada wa habeas," aliandika Pacold, ambaye aliteuliwa na Rais Donald Trump, katika amri ya Alhamisi.
Pacold alisema hoja ya Kelly inaelezea mamlaka ya mahakama kwa njia isiyoeleweka vizuri.