Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, umezuia Mkutano wa waandishi wa habari pamoja na viongozi wa CHADEMA, uliokuwa unatarajiwa kufanyika asubuhi ya saa 5 ya leo Juni 17, katika moja ya ukumbi uliopo kwenye Hotel ya Seashell (Millennium Tower), Makumbusho Dar es Salaam, kwa sababu chama hicho kimezuiwa shughuli za kisiasa.
Aidha Jeshi hilo likawaamuru waandishi wa habari kufunga vifaa vyao na kuondoka eneo hilo Mara moja huku wakibaki na Mkurugenzi wa Mawasiliano na uenezi wa Chama hicho Brenda Rupia.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi wamedai kuwa wamezuia Mkutano huo kwa sababu Chama hicho kimezuiliwa kufanya shughuli zozote za kisiasa.