Trump Alipinga Mpango wa Israel Kumuua Kiongozi wa Iran

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: trump-alipinga-mpango-israel-kumuua-kiongozi-iran-354-rickmedia

Rais wa Marekani Donald Trump alipinga mpango wa Israel katika siku za hivi karibuni wa kumuua Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, maafisa wawili wa Marekani waliliambia shirika la habari la Reuters .

Reuters wanaripoti kuwa Israel ilipata taarifa za alipo kiongozi huyo wa Iran na ilikusudia kutupa makombora lakini Trump alipingana na Israel kwenye hilo.

Trump alisema ana rekodi ya kumaliza mizozo, na kwamba ataifanya Israeli na Iran kusitisha uhasama "kama vile nilivyofanya India na Pakistan kufanya amani" baada ya mzozo wa hivi karibuni wa nchi hizo mbili.