Gavi atua nchini Tanzania kwaajili ya Mapumziko

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 hours ago
rickmedia: gavi-atua-nchini-tanzania-kwaajili-mapumziko-376-rickmedia

Nyota wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania, Pablo Gavi amefuata nyayo za baadhi ya mastaa wa soka wa nchi yake kwa kuja mapumzikoni Tanzania.

Kiungo huyo yupo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti sambamba na mpenzi wake, Ana Pelayo.

Gavi ametua Tanzania ikiwa ni siku chache baada ya nyota wengine watatu wa soka wa Hispania kutembelea hapa nchini kwa ajili ya mapumziko.

Wachezaji hao ni David Raya, David De Gea na Pedri.

Ukiondoa Wahispania hao, pia Tanzania imepokea nyota wengine wawili wa soka ambao ni mshambuliaji mstaafu wa Sweden, Barcelona na AC Milan, Zlatan Ibrahimovic na mshambuliaji wa Girona na Uholanzi, Arnaut Danjuma.