Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Janeth Rithe, ameachiwa kwa dhamana

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

15 hours ago
rickmedia: mwenyekiti-ngome-wanawake-taifa-chama-cha-act-wazalendo-janeth-rithe-ameachiwa-kwa-213-rickmedia

Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Janeth Rithe, ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 23,2025 na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa chama hicho, Shangwe Ayo, Rithe aliachiwa kwa sharti la kuripoti tena kituoni hapo siku ya Jumatano, tarehe 25 Juni 2025.

Hata hivyo, sababu za kushikiliwa kwa kiongozi huyo bado hazikuwa zimewekwa wazi na Jeshi la Polisi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa "Chama kitatoa taarifa zaidi katika wakati muafaka"