Boniface Mwambukusi ashinda Urais wa Chama Cha Wawakili Tanganyika TLS

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

10 months ago
rickmedia: boniface-mwambukusi-ashinda-urais-chama-cha-wawakili-tanganyika-tls-788-rickmedia

 Wakili Boniface Mwabukusi ametangazwa kuwa Mshindi wa Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) akiwashinda Wanasheria wengine watano waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Mwabukusi ameshinda kwa Kura 1,274 huku Sweetbert Nkuba akifuatia kwa Kura 807. Kwa matokeo hayo, Mwabukusi anakwenda kukiongoza Chama hicho cha Wanasheria kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mawakili wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo Kapt. Ibrahim Bendera aliyepata Kura 58, Paul Kaunda aliyepata Kura 51, Emmanuel Muga aliyepata Kura 18 na Revocatus Kuuli aliyepata Kura 7.