Mahakama kuu ya Jamaica imeamuru serikali kumlipa fidia Mzee wa Miaka 76 wa Jamaica, #GeorgeWilliams ya $120M.
Williams alikuwa na umri wa miaka 20 tu alipokamatwa mwaka 1970 kwa tuhuma za mauaji. Mamlaka zilidai hakuwa na uwezo wa kisaikolojia kusimama kizimbani, lakini badala ya kumpatia matibabu au mchakato wa haki, walimtupa tu kama amesahaulika. Aliwekwa gerezani kwa miaka 50, ambapo miaka 42 kati ya hiyo ilipita bila hata mapitio ya kesi yake. Hakukuwa na kesi. Hakukuwa na kusikilizwa. Kimya tu.
Sasa, Jaji #SonyaWintBlair ameagiza serikali ya Jamaica kulipa fidia hiyo. Williams anatarajiwa kupokea Dola milioni 42 kama fidia ya ukiukwaji wa haki zake, na Dola milioni 78 nyingine kama fidia ya mateso na madhila aliyoyapitia.
Wanaharakati waliopigania kuachiliwa kwake wanasema huu ni ushindi wa machungu. Wengine wamedai ni bora kuliko kutopata chochote, wakibainisha kuwa hakuna kiasi cha fedha kinachoweza kumrudishia uhuru wake, ujana wake, wala utulivu wa akili.