Enock Bella amuomba Msamaha Mbosso

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

4 hours ago
rickmedia: enock-bella-amuomba-msamaha-mbosso-195-rickmedia

Msanii aliekuwa anauNDA Kundi la #YaMotoBand, #EnockBella amemuomba Msanii mwenzake #Mbosso waliokuwa pamoja kwenye kundi hilo Msamaha baada ya kumuongelea vibaya kwenye baadhi ya mahojiano yake.

Siku ya jana #Mbosso alifanya mahojiano na Waandishi wa Habari na kusema alisikitishwa na kauli mbalimbali za #EnockBella kuwa hajawahi kumsaidia licha ya kumfanyia mambo mengi kwenye maisha yake.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Ameandika..

"FAMILY FIRST, kaka yangu na ndugu yangu @mbosso_ kwanza nichukue nafasi hii kuomba RADHI hadharani kwa kukukwaza kwenye mahojiano niliyofanya mwaka jana, kama binadamu siwezi kuwa sawa siku zote na ndio ubinadamu kwa hilo nabeba uwajibikaji na naomba RADHI.

Kama ulivyosema ROOM NUMBER MOJA ( YAMOTO BAND) ilikuwa si tu band bali shule nzima ya maisha na viongozi wetu walitufundisha kusaidiana, kuchukuliana madhaifu, kuwajibika na kuomba radhi ukiteleza, hivyo ndugu yangu NIWIE RADHI,

Watanzania wapenzi wa @mbosso_ na @enockbellaofficial nawaomba pia radhi kwa kukwazika sisi bado ni vijana wenu wenye ndoto za kupambania na supporters wetu ni nyie hivyo kwa lilitokea mniwie radhi kijana wenu na muendelee kutupa support na tuendelee kuenjoy miziki mizuri iliyo ndani ya ROOM NUMBER THREE #RN3

Ndugu zangu wa media naomba sana, sitakuwa na mahojiano tena kuhusu suala hili kwangu nimelimaliza hapo , ndugu yangu amesema nilichomkwaza na ninaomba radhi hivyo sina maoni mengine juu ya interview ya kaka yangu @mbosso_ tutafutane kwa maswali mengine ila si kwa swala hili 🙏"