Rais Samia Ni Mgeni Rasmi kwenye Uhuru Wa Msumbiji

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: rais-samia-mgeni-rasmi-kwenye-uhuru-msumbiji-219-rickmedia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili Jamhuri ya Msumbiji 24 Juni 2025 ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, kufuatia mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Daniel Francisco Chapo. Sherehe hizo zinafanyika leo katika Uwanja wa Machava, Mjini Maputo.

Mwaliko huo Kidiplomasia na ushawishi wa nchi nje ya mipaka ya Tanzania, unaonyesha kukubalika kwa Rais Samia na pia kukua kwa diplomasia ya Tanzania mpaka kupewa mwaliko maalum wa kuwa mgeni rasmi wakati nchi nyingine inapoadhimisha sherehe zake za Uhuru. Msumbiji ni taifa kubwa ambalo lina historia kubwa sana Afrika na Duniani, katika ma-rais wote na wageni wote walioalikwa Msumbiji kuchaguliwa Rais Samia kuwa mgeni rasmi kunaonyesha kukubalika kwake katika nchi nyingine lakini pia mchango wake unatambulika hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Katika historia ya Tanzania, akiwa Rais mwanamke wa Kwanza, anakuwa pia Rais ambaye amepata mwaliko maalum wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uhuru ya nchi nyingine. Imezoeleka kwenda kuhudhuria na sio kuwa mgeni rasmi, lakini mara hii ni heshima kubwa sana kwa nchi, kupitia Rais Samia kupata mwaliko rasmi wa kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Uhuru wa nchi nyingine.