Mwanaume mmoja aliekuwa Miongoni mwa Ma-dancer kwenye Show ya Super Bowl HalfTime ambayo Alitumbuiza Rapa #KendrickLamer amekamatwa na Polisi kwa kosa la kuingia na bendera yenye maandishi “Sudan na Free Gaza”
Mamlaka zinasema kuwa #ZulQarnainKwameNantambu mwenye umri wa miaka 41 alikiuka jukumu alilopewa wakati wa onyesho la #Lamar kwa kuingia na kuanza kukimbia na Bendera hiyo ambayo haikuwa kwenye mipango ya onyesho.
Msemaji wa NFL, Brian McCarthy, aliwashukuru wachunguzi kwa kazi yao.
"Tunachukulia kwa uzito mkubwa jaribio lolote la kuvuruga sehemu yoyote ya mchezo wa NFL, ikiwa ni pamoja na onyesho la mapumziko ya kipindi, na tunafurahi kwamba mtu huyu atawajibishwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria," McCarthy alisema katika taarifa.