Staa wa Muziki #Mbosso amkunjulia Moyo Msanii mwenzake #EnockBella baada ya kumuomba Msamaha.
#Mbosso ametoa Stori fupi ya wao wawili..
"Kipindi Wenzetu Wawili Wametangulia Kupata Management na Kuachia Kazi Zao na Wakiwa Wanafanya Shows zao .. Mimi na Wewe Ndo Tulikuwa Tunaongea Muda Mwingi ndani pale Maskani Tabata Savanna…
Niliacha Mziki na Sikuwa Nataka Mziki Kabisa Baada ya Kuona Ya Moto Band imevunjika .. ila Siku niliokukuta Unalia Chumbani Peke Yako na Ukasema ‘ Nakunukuu “.. Mbosso Fanya Mziki Wewe Utanisiadia Naujua Moyo Wako ..” Nilikusikiliza na niliamua Kuanza Tena Mishe mishe Za Miziki na kwa Baraka Za Mungu Neema zilianza na nilichagua kushare na wewe Kwenye Kidogo na Kikubwa nilichopata ..,
Nilifanya Hivyo Kaka Kuanzia Kwenye Shows zangu Hadi Kwenye Maisha Ya Kawaida Kwa Ujumla … Unajua Kwa Nini …? Kwa Sababu Kauli Yako Moja ilitosha Sana Kunipa ujasiri na Leo Nipo Hapa …
Love You so Much Bro ❤️🫂"