Nyota wa Liverpool, DiogoJota (28) amefariki Dunia kutokana na ajali ya gari iliyotokea Nchini Uhispania ikiwa ni wiki mbili tangu afunge ndoa na Rute Cardoso, ambapo Wanandoa hao wana Watoto watatu.
Taarifa zinaeleza ajali hiyo imetokea wakati akisafiri kwa gari akiwa na mdogo wake Andre (26) ambaye naye amepoteza maisha baada gari lao kuacha njia, na kwenda kugonga sehemu na kisha kuwaka moto.
Winga huyo raia wa Ureno enzi za uhai wake alipata nafasi ya kucheza katika timu kadhaa; Paços de Ferreira, Atlético Madrid, Porto, Wolverhampton Wanderers kisha akatua Liverpool Mwaka 2020.
-