Kanye West Apigwa Marufuku Kuingia Australia

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: kanye-west-apigwa-marufuku-kuingia-australia-945-rickmedia

Rapa wa Kimarekani #KanyeWest amezuiliwa kuingia Australia kutokana na wimbo unaomsifu #AdolfHitler.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Australia, #TonyBurke, amefichua kuwa wizara yake imefuta visa halali ya #West baada ya kutolewa kwa wimbo #HeilHitler mapema mwezi Mei.

Wimbo huo wa #West umelaaniwa vikali na umepigwa marufuku kwenye majukwaa mengi ya kidijitali.

Rapa huyo mwenye utata mkubwa, amekuwa akitoa matamshi ya chuki dhidi ya Wayahudi. Ameoa mbunifu wa mavazi kutoka Australia, #BiancaCensori.

Bw. Burke alifichua hatua ya kufuta visa hiyo alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Australia (ABC), katika mjadala kuhusu mtu mwingine ambaye pia alinyimwa visa kwa matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu.

"Kama mtu angehoji kuwa chuki dhidi ya Wayahudi ina mantiki, nisingemruhusu kuingia hapa," alisema Bw. Burke alipomzungumzia West.

"[West] amekuwa akija Australia kwa muda mrefu na ametoa matamshi mengi ya kuudhi.

"Lakini maafisa wangu walipitia tena kesi yake baada ya kutoa wimbo Heil Hitler, na sasa hana tena visa halali ya Australia."

Haijabainika wazi iwapo West amepigwa marufuku kabisa kuingia Australia. Bw. Burke alisema kuwa maombi ya visa yatapitiwa upya kila mara yanapowasilishwa, kulingana na sheria za Australia.

Lakini alipoulizwa kama marufuku yoyote dhidi ya West inaweza kudumu, Bw. Burke alisema:

"Nadhani kisichoweza kudumishwa ni kuingiza chuki... Tayari tuna matatizo mengi nchini bila kuleta ubaguzi kwa makusudi."

Sio mara ya kwanza kwa Australia kufikiria kumzuia West. Mwaka 2023, Waziri wa Elimu wa Australia, Jason Clare, pia alilaani matamshi ya West kuhusu Hitler na mauaji ya Holocaust, na akapendekeza kwamba angeweza kunyimwa visa.