Samuel Eto’o apigwa faini ya Tsh.Milioni 51, matendo yake ya AFCON Morocco chanzo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: samuel-etoo-apigwa-faini-tshmilioni-51-matendo-yake-afcon-morocco-chanzo-135-rickmedia

Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto’o amefungiwa mechi nne na kulipishwa faini ya dola za Marekani 20,000 (sawa na shilingi milioni 51 za Tanzania).

Faini hiyo ni Kutokana na matendo yake wakati wa mechi ya Nusu fainali ya AFCON 2025 dhidi ya Morocco.

Eto’o alipinga maamuzi ya waamuzi uwanjani, na kusababisha CAF kuchukua hatua hiyo.

FECAFOOT imesema kuwa itaomba rufaa dhidi ya uamuzi huo, ikidai kuwa mchakato ulofuatwa ulikuwa wa haraka na haukuwa na uwazi.