Mapema leo hii Mbunge wa Kigoma Mjini Clinton Revocatus Chipando maarufu kama Babalevo amemnunua zawadi ya gari aina ya Range ;over mke wake (Mama Ruby), hii ni kama sehemu ya Babalevo kutoa shukrani zake kwa Mama Ruby kwa kumvumilia siku zote na kuwa upande wake nyakati zote.
Mama Ruby ameipokea zawadi hiyo kwa mikono miwili huku akionyesha moyo wake wa shukrani kwa mume wake pamoja na kuweka utani kwa mashabiki zake kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuwaambia wampishe njia mama mheshimiwa anapita.
Diamond na Zuchu ni watu wa karibu wa familia hii ya Babalevo na nimeona wote wawili wakiacha maoni yao kumpongeza Mama Ruby kwa uvumilivu huku wakisisitiza kuwa anastahili zawadi hiyo kwa uvumilivu wake.

Babalevo naye anakiri wazi kuwa mke wake huyo aliyeishi naye kwa miaka 10 amevumilia mengi kuishi na yeye kwani ni kazi nzito, anasema anamshangaa mkewe amewezaje kwenye hilo na katika kuhakikisha mkewe anajua kuwa anamshukuru basi mwaka huu 2026 atahakikisha anatembelea nchi 29 duniani.
Hakika Mama Ruby anastahili zawadi hii na zaidi kutoka kwa mumewe ,hongera sana Babalevo kwa kuzidi kuikumbuka familia yako.