Zuchu amnunulia Mama yake (Bi. Hadija Kopa) gari aina ya Prado

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 hours ago
rickmedia: zuchu-amnunulia-mama-yake-bi-hadija-kopa-gari-aina-prado-559-rickmedia

Msanii Zuchu ameamua kuonyesha furaha ya kipekee ya mama yake baada ya kumzawadia mama yake (Bi.Khadija Kopa) gari aina ya Prado. Sasa kwenye video aliyoipost ameonyesha mapokezi ya mama yake, Zuchu alidai kwamba mama yake hakulala usiku kutokana na furaha kubwa baada ya kushuhudia zawadi hiyo.

Hii sio gari ya kwanza Zuchu kumnunulia mama yake, mara ya kwanza alimnunulia gari aina ya Alphad na ndio hiyo ambayo kwenye video Zuchu anasema kuwa Bi.Khadija Kopa alikuwa akimwambia amnunulie gari nyingine maana hIyo school bus ameichoka.

Bi Hadija Kopa sio mtu pekee kwenye sanaa aliyewahi kununuliwa gari na Zuchu, msanii Anjella pia aliwahi kuzawadiwa gari aina ya Subari na Zuchu kama sehemu ya kumsapoti msanii mwenzake wa kike.

Tazama Hapa Chini 👇🏽