Mastaa mbalimbali walivyojitoa kumtetea Diamond kuhusu kumsaidia Mkubwa Fella

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

23 hours ago
rickmedia: mastaa-mbalimbali-walivyojitoa-kumtetea-diamond-kuhusu-kumsaidia-mkubwa-fella-316-rickmedia

Kumekuwa na vuta nikuvute kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wasanii kuto kutoa msaada kwa Meneja mkubwa nchini Said Fell maarufu kama Mkubwa Fella huku chanzo chake kikiwa kinatoka kwa mke wake Sweet Fella baada ya kuwalalamikia wasanii kuto kumsaidia mumewe huku akisema Diamond Platnumz kwasasa hapokei simu wakimpigia kwaajili ya msaada.

Watu mbalimbali wameshangazwa na familia ya Fella kulalamika kutosaidiwa na wasanii huku wakimshangaa zaidi kwa kumlaumu Diamond Platnumz kwani ndiye msanii aliyewasaidia sana tangu changamoto hii impate mpendwa wao

Mama mzazi wa Diamond Platnumz Bi.Sandra maarufu kama Mama Dangote naye pia ametoa ya moyoni kwenye sakata hili huku akisisitiza kuwa yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kupigiwa na mke wa Fella kwani Diamond hakuwa nchini na alipokwenda kumuona Diamond limuomba ampatie Milioni 5 siku ya kwanza kabisa.

Msanii Faiza Ally pia amesikitishwa na jambo hilo na amejikuta akipost kusisitiza kuwa Diamond Platnumz hakuzaliwa ili aje kutoa msaada duniani.

Dada wa Diamond Platnumz yeye pia amemtaka mdogo wake kumuachia Mungu jambo hili kwani binadamu hawana shukrani siku zote.

Dudu Baya pia kwenye baadhi ya mahojiano aliyofanya na vyombo mbalimbali vya habari alishangazwa na namna ambavyo familia ya Fella inatupa lawama kwa wasanii kuto kumsaidia Fella huku akisema mambo ambayo yeye pia anaamini yuko sawa kwa upande wake.

Wapo watu wengi waliozungumzia sakata hili lakini kubwa na la msingi ni kumuombea mzee wetu Said Fella (Mkubwa Fella) aipambanie afya yake na arudi ili aendelee na majukumu yake kama kawaida na watu waache kunyoosheana vidole amani izidi kutawala.

Get Well Soon Mkubwa Fella