Rihanna huenda anawaza kuongeza mtoto wa nne mwaka 2026 baada ya kuibua gumzo kubwa mitandaoni. Mwanamuziki na mfanyabiashara wa Fenty aliweka maoni ya video maarufu Instagram iliyokuwa ikiuliza mtu achague kati ya “kurudi kuwa hot na sexy” au “kupata ujauzito mwaka ujao,” na majibu yake yaliashiria wazi kuwa yupo tayari kwa wazo hilo.
Haya yanajiri miezi michache tu baada ya Rihanna na mwenza wake A$AP Rocky kumkaribisha mtoto wao wa tatu. Licha ya mashabiki kuendelea kusubiri kwa hamu muziki mpya, Rihanna anaonekana kufurahia zaidi mazungumzo ya uzazi na safari ya kuwa mama.
Kwa sasa hakuna tangazo rasmi, lakini kama kawaida yake, kauli ndogo ya Rihanna imetosheleza kuwasha kutengeneza mjadala mkubwa duniani