Brighton & Hove Kuachana na Aisha Masaka mwisho wa msimu

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: brighton-hove-kuachana-aisha-masaka-mwisho-msimu-985-rickmedia

Klabu ya Brighton & Hove Albion inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini England haitaendelea na mshambuliaji wa Kitanzania, Aisha Masaka, msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Tangu ajiunge na timu hiyo msimu wa 2023/24 akitokea BK Hacken ya Sweden, nyota huyo alicheza mechi mbili kwa dakika 14 dhidi ya Arsenal (4) na Birmigham (10).

Sababu kubwa za Brighton kuchukua uamuzi huo zinatajwa kuwa ni kiwango ambacho mchezaji huyo amekionyesha pamoja na changamoto ya majeraha yaliyomsumbua kwa nyakati tofauti tangu ajiunge na klabu hiyo, hali iliyomfanya ashindwe kuwa na mwendelezo bora.

Straika huyo wa zamani wa Yanga Princess, alijiunga na Brighton akitarajiwa kuleta ushindani katika safu ya ushambuliaji, hata hivyo hali haikuwa rahisi kwake kutokana na majeraha pamoja na ushindani mkubwa wa nafasi ndani ya kikosi hicho.