Gari ya Mbunge wa Kigoma Mjini aina ya Jeep Wrangler aliyoinunua kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kwenye shughuli za harusi, imepata ajali mbaya usiku wa kuamkia leo ikiwa njiani kutoka Kigoma kuelekea Dodoma majira ya saa 6 usiku.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa, dereva wa gari hilo yuko salama, ingawa gari limeharibika vibaya baada ya kupinduka katika ajali hiyo.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Clinton Revocatus Chipando maarufu kama Babalevo amethibitisha tukio hilo kupitia mitandao ya kijamii na kuonesha masikitiko yake, akisema:
“Alichopanga Mungu, hakuna anayeweza kupangua.”
Tunaendelea kufuatilia kwa karibu ili kupata taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo.