Mr.Beast analalamika kuwa kuna kipindi hukosa pesa kabisa licha ya umilionea

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: mrbeast-analalamika-kuwa-kuna-kipindi-hukosa-pesa-kabisa-licha-umilionea-337-rickmedia

YouTuber maarufu wa Marekani, MrBeast (Jimmy Donaldson), amefichua kwamba licha ya kutajwa kuwa bilionea, akaunti yake binafsi kwa sasa haina pesa kabisa, na anadaiwa kuomba mkopo kutoka kwa mama yake, ili kulipa baadhi ya gharama za maisha.

MrBeast ameleza kuwa mapato yake mengi huwekezwa tena kwenye biashara na videos zake, ikiwemo Beast Industries na Feastables, jambo ambalo linamfanya awe na pesa kidogo. Anasema kwamba mara nyingi hujilipa kiasi kidogo cha kutosha kwa matumizi ya kila siku, huku mamilioni ya dola zikielekezwa kwenye miradi ya video na biashara zake.

Hata hivyo, kwenye vyombo vya habari, thamani yake ya utajiri inakadiriwa kuwa bilionea, kutokana na umiliki wa kampuni zake, lakini hiyo haimaanishi ana pesa nyingi benki. MrBeast anaweka wazi kuwa tajiri, hakuendi sambamba na kuwa na pesa nyingi za kutumia.