Nyota wa Soka Ka kulipwa , #ThomasPartey, amefunguliwa mashtaka ya ubakaji mara tano na unyanyasaji wa kingono mara moja.
Polisi wa Metropolitan wamesema makosa hayo yanadaiwa kutokea kati ya mwaka 2021 hadi 2022.
Mashtaka hayo yanahusisha wanawake watatu, ambapo makosa mawili ya ubakaji yanahusiana na mwanamke mmoja, makosa matatu ya ubakaji yanahusiana na mwanamke wa pili, na kosa moja la unyanyasaji wa kingono linahusiana na mwanamke wa tatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ghana amekanusha mashtaka yote na kupitia wakili.
Mkataba wa Partey na Arsenal ulimalizika siku ya Jumatatu baada ya kuchezea timu hiyo tangu mwaka 2020.
Mashtaka hayo yamefuatia uchunguzi wa muda mrefu uliofanywa na maafisa wa upelelezi, ambao ulianza Februari 2022 baada ya kupokea taarifa ya awali ya ubakaji.
Kamishna Msaidizi Andy Furphy, anayeongoza uchunguzi huo, alisema: “Kipaumbele chetu kinabaki kuwa kuwapa msaada wanawake waliojitokeza.
“Tunaomba yeyote aliyeathiriwa na kesi hii au mwenye taarifa zozote kuwasiliana na timu yetu”
Partey, mkazi wa Hertfordshire, anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Westminster Magistrates tarehe 5 Agosti.
Katika taarifa, wakili wake Jenny Wiltshire alisema: “Thomas Partey anakana mashtaka yote dhidi yake.