Rais wa Senegal atangaza mapumziko kufuatia ushindi wao AFCON

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

20 hours ago
rickmedia: rais-senegal-atangaza-mapumziko-kufuatia-ushindi-wao-afcon-902-rickmedia

Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ametangaza Jumatatu, Januari 19, 2026, kuwa sikukuu ya kitaifa ili kuenzi ushindi wa timu ya taifa kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, baada ya Senegal kushinda 1–0 dhidi ya Morocco katika mchezo uliofanyika Rabat.

Hii ni mara ya pili Senegal kutwaa ubingwa wa AFCON. Rais Faye amewataka raia kusherehekea mafanikio hayo na pia ameahidi zawadi za kifedha kwa wachezaji na benchi la ufundi.