Kibabage asajiliwa Simba Sports Club bila malipo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

10 hours ago
rickmedia: kibabage-asajiliwa-simba-sports-club-bila-malipo-91-rickmedia

Singida Black Stars imetangaza kuwa beki wake Nickson Kibabage amejiunga na Simba kwa uhamisho wa bure baada ya makubaliano baina ya pande hizo.

Taarifa iliyotolewa na Singida Black Stars leo, imefafanua kuwa klabu hiyo imeridhia Kibabage ajiunge na Simba kwa faida ya mchezaji husika.

“Singida Black Stars inapenda kuufahamisha umma kuwa imekubali maombi kutoka kwa uongozi wa Klabu ya Simba ya kumruhusu mchezaji Nickson Kibabage kujiunga na klabu hiyo.

“Baada ya majadiliano, uongozi umeamua kumtoa mchezaji huyo bila malipo.

Singida Black Stars inaamini katika falsafa ya uendelezaji vipaji hasa kwa wachezaji wazawa. Uongozi wa klabu umeona hii ni fursa nzuri kwa mchezaji mzawa kwa kuwa Simba SC inashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Nickson Kibabage ni Mchezaji wa Timu ya Taifa.