Jeshi la Polisi Uganda limekanusha taarifa zinazosambaa kuwa mgombea urais wa upinzani, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine), alitekwa na kupelekwa kusikojulikana, likizitaja kama za kupotosha na uchochezi.
Hata hivyo, chama chake cha National Unity Platform (NUP) kinasema Bobi Wine alichukuliwa kwa nguvu nyumbani kwake na watu wanaodaiwa kuwa wanajeshi na kusafirishwa kwa helikopta ya kijeshi kwenda eneo lisilojulikana.