Klabu ya Simba Sc imewataka mashabiki wake walionunua tiketi kwa ajili ya mchezo wa fainali Kufanya hivi

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

10 hours ago
rickmedia: klabu-simba-imewataka-mashabiki-wake-walionunua-tiketi-kwa-ajili-mchezo-fainali-kufanya-789-rickmedia

Klabu ya Simba Sc imewataka mashabiki wake walionunua tiketi kwa ajili ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika katika ambao awali ilidhaniwa ungechezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa wazitunze tiketi hizo kwa ajili ya kuzitumia kwenye Simba Day.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally ametangaza utaratibu mpya wa viingilio kuelekea mchezo huo ambao sasa utachezwa katika dimba New Amaan, Complex Zanzibar.

Viingilio katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar vitakuwa Tsh 50,000 kwa VIP, Tsh 30,000 kwa URUSI na Tsh 10,000 kwa mzunguko.

“Mchakato wa uuzwaji wa Tiketi umeanza upya, hivyo wale wote ambao mlinunua Tiketi zitunzeni mtazitumia siku ya Simba Day.___ Kauli ya Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally akizungumza na wanahabari.