Kesi ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu upelelezi haujakamilika, yaahirishwa hadi Mei 19, 2025

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: kesi-uhaini-dhidi-tundu-lissu-upelelezi-haujakamilika-yaahirishwa-hadi-mei-19-2025-178-rickmedia

Shauri la Kwanza la Uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA – Taifa, Tundu Lissu limeahirishwa mpaka Mei 19, 2025, huku Mahakama ikiutaka upande wa Jamhuri uharakishe upelelezi.

Ikumbukwe kuwa wakati mshtakiwa akifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa shtaka la uhaini kwenye kesi ya kwanza, upande wa mashtaka ulieleza kwamba bado upelelezi wa kosa hilo ulikuwa bado haujakamilika.

Mchakato wa kesi hiyo unaendelea leo Mei 6, 2025 kwa njia ya Mtandao. Mwanasiasa huyo anakabiliwa na tuhuma mbili ambazo ni Uhaini na Kutoa Taarifa za Uongo.