Mwimbaji kutoka nchini Marekani, Alicia Keys, amethibitisha kuwa thamani ya familia kwake ni kubwa kuliko fedha, baada ya kukataa ofa nono ya dola milioni 9 sawa na Tsh Bilioni 24 kwa ajili ya kutumbuiza kwa dakika tisa pekee.
Kwa mujibu wa mume wake, Swizz Beatz, kampuni moja ilimpatia ofa hio nono lakini Alicia alikataa bila kusita na kuchagua kutumia muda huo kuwa pamoja na mumewe. Swizz Beatz aliongeza kuwa hata kama wangetoa dola milioni 100, Alicia bado hasingekubali kubadili uamuzi wake.