Wizara ya Afya nchini imetangaza ongezeko la watu wenye maambukizi ya ugonjwa wa Uvi-ko-19 nchini katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Mganga Mkuu wa serikali Dk Grace Magembe amesema kumekuwepo na ongezeko la tetesi zinazo-husiana na magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa katika jamii hapa nchini.
“Hali ya kuongezeka na kupungua kwa ugonjwa huu imekuwepo kila mwaka tangu kutangazwa kwa ugonjwa huu mwaka 2020. Kwa kipindi hiki ongezeko hili linaonekana zaidi katika Mkoa wa Dar es Salaam,” amesema Dk Magembe.
Wananchi wametakiwa kuzingatia kanuni za afya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maam-bukizi ya magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa.