Bodi ya Filamu Tanzania imemtaka Staa wa Movie Bongo #WemaSepetu kufika katika ofisi zao kwa ajili ya mahojiano baada ya picha jongevu zilizotafsiriwa kutokuwa na maadili kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha #WemaSepetu akiwa kwenye mavazi yasiyo na Stara.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa:
"Bodi ya Filamu ni chombo kilichoundwa kisheria kwa ajili ya kutengeneza na kulinda taswira ya taifa letu pamoja na kuendeleza sekta ya filamu nchini. Katika kutekeleza jukumu hilo, Bodi haiwezi kuacha kusimamia masuala ya nidhamu na maadili kwa wanatasnia wetu."
Aidha, Bodi imetoa wito kwa wasanii wote nchini kuendelea kulinda maadili ya Taifa si tu kupitia kazi zao za sanaa bali pia katika mienendo yao ya kila siku kwenye jamii.