Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amesema Chama chake kiitwacho ‘Democracy for the Citizens Party (DCP)’ kinalenga ujumuishaji na kina Wanachama wa makundi yote wakiwemo GenZ.
Gachagua pia alitaja Viongozi wa Chama hicho wakiwemo David Mingati (Mwenyekiti), Cleophas Malala (Naibu Kiongozi wa Muda wa Chama) na Cate Waruguru (Kiongozi wa Wanawake).
Aidha, Gachagua ametangaza kuwa Chama hicho kitazinduliwa rasmi Juni 4, na baadaye ataanza ziara ya Miaka Miwili kote nchini kueneza Sera za chama na kuomba uungwaji mkono. Pia, amewataka wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa 2026 kupitia Chama hicho kuanza kujisajili.