Polisi wa Metropolitan wametoa taarifa kuwa Mwanamuziki wa Marekani #ChrisBrown ameshtakiwa kwa kosa la kusababisha madhara makubwa ya mwili Baada ya kumshambulia mtu kwa makusudi.
Shtaka hilo linahusiana na madai ya shambulio kwa chupa lililotokea katika Club ya usiku mjini London mwaka 2023.
#Brown bado anashikiliwa na anatarajiwa kufikishwa Mahakamani.
Kwa sasa yuko kwenye ziara ya muziki na amepanga kufanya maonyesho kadhaa nchini Uingereza mwezi Juni na Julai.