Mahakama Yamnyima Dhamana Chris Brown

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: mahakama-yamnyima-dhamana-chris-brown-832-rickmedia

Staa wa Muziki #ChrisBrown amenyimwa dhamana na mahakama ya Uingereza na atazuiliwa rumande hadi Juni 13 baada ya kufunguliwa mashtaka ya shambulio kutokana na tukio lililotokea kwenye Club.

Msanii huyo wa R&B mwenye umri wa miaka 36 anashtakiwa kwa kosa la kusababisha madhara makubwa kwa mtu baada ya kumpiga Chupa wakiwa Club na Alifikishwa katika Mahakama ya Manchester Magistrates.

Shambulio hilo linadaiwa kutokea katika eneo la burudani lililopo Hanover Square, London mnamo Februari 19, 2023, na linamhusisha mtayarishaji wa muziki aliyeshambuliwa.

Brown alikamatwa na Polisi wa Jiji la London (Metropolitan Police) huko Manchester siku ya Alhamisi.

Anatarajiwa kufanya maonyesho kadhaa nchini Uingereza kama sehemu ya ziara yake ya kimuziki. Kesi yake imehamishiwa katika Mahakama ya Southwark Crown mjini London, ambako atafikishwa tena Juni 13.