Simba Wachachamaa Mechi Yao ya Fainali Kupelekwa Zanzibar

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

4 weeks ago
rickmedia: simba-wachachamaa-mechi-yao-fainali-kupelekwa-zanzibar-564-rickmedia

Zipo taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mchezo wa fainali ya pili ya kombe la Shirikisho Afrika utapigwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar badala ya uwanja wa Benjamin Mkapa tofauti na wengi walivyotarajia

Fununu hizo zimeenda mbali na kubainisha kuwa Shirikisho la soka Afrika (CAF) limeliagiza Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuhamishia maandalizi ya mechi hiyo Zanzibar baada ya CAF kutoridhishwa na maboresho yaliyofanyika kwa Mkapa.

Taarifa hizo zimemuibua Mjumbe Bodi ya Wakurugenzi Simba Sc, Crescentius Magori ambaye amehoji uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar unabeba watu 15000 na tayari Simba Sc imeuza tiketi 12000 kuelekea mchezo na kuisihi CAF kuurejesha mchezo huo kwa Mkapa kuepuka fujo na machafuko.

Katika chapisho lingine Magori amemsihi Rais wa CAF, Patrick Motsepe kuwa uwanja wa Mkapa upo kwenye hali nzuri huku akienda mbali na kumtahadharisha Rais Motsepe kuwa makini watu wake wanamdanganya. “Tunajua Berkane inamilikiwa na nani, lakini kama Simba Sc na Watanzania hayupo tayari kwa hili”— ameandika Magori

Ikumbukwe Mmiliki wa klabu ya RS Berkane, Fouzi Lekjaani Makamu wa Rais wa CAF na ni Rais wa shirikisho la mpira Morocco na anahusika sana na maamuzi mengi kwenye mpira wa Africa.

Licha taarifa za mchezo huo kuchezwa Zanzibar kusalia kama fununu tu lakini inaelezwa kuwa tayari klabu ya RS Berkane imeweka 'oda' ya hoteli watakayofikia Zanzibar tangu juzi kuelekea mchezo huo

Hata hivyo kupitia ukurasa wake rasmi wa mitandao ya kijamii, Simba Sc imeandika Taarifa rasmi kuhusu uwanja wa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itatolewa baada ya mchezo wa awali utakaochezwa Jumamosi Mei 17, 2025.”