Kulingana na #Bloomberg, Utajiri wa #ElonMusk umepungua kwa dola bilioni 34 (Trilioni 88+) ikiwa ni mojawapo ya hasara kubwa zaidi ya siku moja kwa mtu binafsi.
Hasara hiyo iliongezeka kufuatia mfululizo wa machapisho kwenye mtandao wa X kutoka kwa #Musk, akidai kwamba Rais #DonaldTrump alikuwa na uhusiano na marehemu #JeffreyEpstein na kupendekeza kwamba alimsaidia #Trump kushinda uchaguzi wa 2024.
Kwa kujibu, .Trump alitishia kukata mikataba ya serikali na kampuni za Musk na kuondoa msamaha wa ushuru wa magari ya umeme (EV) uliokuwa umeanzishwa chini ya utawala wa Rais wa zamani Joe Biden kupitia Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei ya mwaka 2022, iliyotoa hadi dola 7,500 kama punguzo kwa ununuzi wa magari ya umeme, jambo ambalo lilinufaisha Tesla na kuipa nafasi ya juu kwenye soko la Marekani.