Mwanamuziki kutoka Nchini Tanzania Lavalava ameondoa rasmi utambulisho wa kuwa chini ya lebo ya WCB Wasafi katika ukurasa wake wa Instagram na kudhihirisha kuwa kwa sasa amemalizana na Lebo.
Tukumbuke siku chache hapo nyuma Staa wa muziki Diamond Platnumz alizungumza na Waandishi wa habari na kudai kuwa kama Lavalava atahitaji kutoka kwenye lebo yake atamruhusu na hatomtoza hata senti mia kwani ni miongoni mwa wasanii waliomuonyesha ni dhamu kubwa sana.