Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Rais wa Marekani, #DonaldTrump, yuko tayari kukutana na Rais wa Urusi, #VladimirPutin, na Rais wa Ukraine, #VolodymyrZelensky, nchini Uturuki, wakati juhudi za kufikia usitishaji mapigano zikiendelea.
Ingawa wajumbe kutoka pande zote mbili hawakufikia makubaliano katika mazungumzo yao ya hivi karibuni yaliyofanyika Istanbul, walikubaliana juu ya kubadilishana wafungwa kwa kiwango kikubwa. Rais wa Uturuki, #RecepTayyipErdogan, amependekeza raundi ya tatu ya mazungumzo ya juu baadaye mwezi huu, yafanyike aidha Istanbul au Ankara, yakiwahusisha Trump, Putin, na Zelensky.
Putin hadi sasa amekataa mwaliko huo, huku Zelensky akieleza kuwa yuko tayari, akisema kuwa masuala nyeti yanaweza tu kutatuliwa katika ngazi ya viongozi.
Zelensky, akizungumza baada ya mazungumzo, alimhimiza Trump kuchukua hatua kali zaidi na kuongeza vikwazo dhidi ya Urusi ili kuhimiza usitishaji mapigano wa kudumu. Alisisitiza kuwa mvamizi hastahili kupewa zawadi kwa vita.