Zaidi ya watu 60 wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya waasi wa ADF wanaoungwa mkono na ISIS kushambulia kwa mapanga wakati wa mazishi katika mji wa Ntoyo, Lubero – Kivu Kaskazini.
Afisa wa eneo hilo Macaire Sivikunula na Kamanda wa Kijeshi Kanali Alain Kiwewa wamesema idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwani wengine bado hawajapatikana.
ADF ni miongoni mwa makundi yenye silaha yanayohangaisha mashariki mwa Kongo, eneo tajiri kwa madini.