Auawa Baada ya Kukutwa na Mke wa Jirani yake

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: auawa-baada-kukutwa-mke-jirani-yake-906-rickmedia

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia kijana James Nyakoro Kirauka (20), mkulima na mkazi wa mtaa wa Medical Research, kata ya Kitangili, wilaya ya Ilemela kwa tuhuma za mauaji ya Yoel Charles (28), ambaye pia alikuwa mkulima na mkazi wa eneo hilo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi ilitolewa leo kwa waandishi wa habari tukio hilo la kusikitisha lilitokea Julai 16, 2025 saa 3:15 usiku ambapo mtuhumiwa alidaiwa kumchoma na kitu chenye ncha kali marehemu mara tatu katika ubavu wa kushoto tukio lililosababisha majeraha makubwa yaliyompelekea kufariki dunia siku iliyofuata huku chanzo ikidaiwa ni wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea baada ya mtuhumiwa kumfumania marehemu akiwa chumbani kwake na mke wake aitwaye Diana Amos (20), mjasiriamali na mkazi wa mtaa huo huo wa Medical Research ambapo inadaiwa kuwa marehemu na mtuhumiwa walikuwa wanaishi kwenye nyumba moja kama wapangaji.

"Mtuhumiwa James Nyakoro Kirauka alitenda kosa hilo kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali Yoel Charles katika ubavu wake wa kushoto mara tatu na kupelekea kumjeruhi vibaya, baada ya kumfumania akiwa na mke wake aitwaye Diana Amos, miaka 20, msukuma, mkristo, mjasiriamali na mkazi wa mtaa Medical Research, kata ya Kitangili, wilaya ya Ilemela, wakiwa chumbani kwa mtuhumiwa James Nyakoro Kirauka, ambapo yeye na Yoel Charles waliishi nyumba moja na wote walikuwa ni wapangaji katika nyumba hiyo," imesema taarifa hiyo.

"Baada ya tukio hilo majirani walifika kwaajili ya kutoa msaada na hatimaye taarifa zilifika katika kituo cha polisi Kirumba na majeruhi alipelekwa katika hospitali ya rufaa Sekou-toure kwa ajili ya kupatiwa matibabu, wakati madaktari wanajaribu kuokoa maisha yake leo tarehe 17.05.2025, saa 7.30hrs alifariki dunia. Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi,".Imesema taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi.