Serikali ya Nepal imeondoa rasmi marufuku ya mitandao ya kijamii

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: serikali-nepal-imeondoa-rasmi-marufuku-mitandao-kijamii-227-rickmedia

Serikali ya Nepal imeondoa rasmi marufuku ya mitandao ya kijamii iliyowekwa Septemba 4, 2025, baada ya maandamano makubwa yaliyopelekea vifo vya angalau watu 19 na mamia kujeruhiwa. 

Marufuku hiyo ilihusu majukwaa 26 ikiwemo Facebook, Instagram, WhatsApp, YouTube na X, hatua iliyozua hasira kubwa hasa miongoni mwa vijana wa kizazi cha “Gen Z” waliopinga ufisadi na kudai uhuru wa kujieleza. 

Baada ya shinikizo, Baraza la Mawaziri la Dharura liliamua kuondoa marufuku hiyo, huku mawaziri kadhaa wakiwemo wa Mambo ya Ndani, Kilimo na Afya wakiwajibika kwa kujiuzulu. 

Serikali imeahidi fidia kwa familia za wahanga, matibabu bure kwa majeruhi na uchunguzi wa kina ndani ya siku 15. Hata hivyo, maandamano yanaendelea, yakichukua sura ya vurugu zaidi kutokana na hasira za wananchi dhidi ya ukosefu wa ajira, ufisadi na ukandamizaji wa uhuru wa raia.