Ryan W. Routh, mwanaume mwenye umri wa miaka 59, Jana Jumatatu, Septemba 8, alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka matano ya shambulio la jaribio la kumuua Donald Trump. Inadaiwa kuwa Septemba 2024, Routh alijificha na bunduki karibu na uwanja wa gofu wa Trump huko Florida kwa nia ya kumuua Trump alipokuwa akicheza gofu.
Routh ameamua kujitetea mwenyewe mahakamani na amekuwa akitoa hoja zisizo za kawaida, kama pendekezo la kupigana na Trump ("beatdown session"), na ombi la kubadilishwa na mfungwa kutoka China au Iran. Jaji Aileen Cannon, aliyeteuliwa na Trump, amekataa maombi hayo.