Dhamana Ya Lil Durk Ya Bilioni 11 Yakataliwa na Mahakama

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 day ago
rickmedia: dhamana-lil-durk-bilioni-yakataliwa-mahakama-474-rickmedia

Msanii wa muziki wa rap #LilDurk bado yuko kizuizini baada ya Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Marekani kukataa pendekezo lake la dhamana ya dola milioni 4.5, akisema kuwa kiasi hicho hakitoshi kuhakikisha kuwa atahudhuria kesi yake.

Jaji pia alieleza kuwa waendesha mashtaka hawajawasilisha ushahidi wa kutosha kuhalalisha kumweka jela kabla ya kesi.

#Durk anakabiliwa na mashtaka ya shirikisho yanayohusiana na njama ya mauaji kwa malipo inayodaiwa kulenga msanii mwenzake wa rap, #QuandoRondo, ambayo ilisababisha kifo cha binamu yake #Rondo, Saviay’a “#LulPab” Robinson, mwaka 2022. Amejibu mashtaka hayo kwa kusema si hausiki na anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani ikiwa atapatikana na hatia. Kesi hiyo imepangwa kuanza Oktoba 14, 2025.