Rapa #BhadBhabie yupo kwenye ugomvi mzito wa wazi na mama yake, #BarbaraBregoli Akimtaka aache kufuatilia maisha yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Alishare ujumbe mzito akitaja baadhi ya vitu vya thamani alivyompa Mama yake na kumwambia aache kumfuatilia kwani ameshakuwa mtu mzima.
“Nilikununulia nyumba, una magari mawili ya Benz, na Bentley moja. Bado uko kwenye malipo yangu ACHA KUINGILIA MAISHA YANGU, acha kutesa mimi na marafiki zangu na acha kusambaza uongo kwa vyombo vya habari kwa sababu umekasirika.”
#Bhabie aliendelea kusema kuwa mama yake hawezi tena kumdhibiti na kumshauri akubaliane na hilo
“Tafadhali acha kuingilia maisha yangu Barbara,” alihitimisha.
Huu si mzozo wao wa kwanza Uhusiano wa Bhad Bhabie na mama yake umekuwa na misuguano ya muda mrefu wameshakuwa na matatizo ya kisheria, tofauti kuhusu haki za kazi, na hata mambo ya kiafya kuwa hadharani.
Kwa sasa, #BhadBhabie pia ana changamoto nyingine Kesi ya madai ya deni kutoka American Express kwa madai ya kutolipa deni la zaidi ya $674,452 (sawa na zaidi ya TSh 1.7 bilioni).