HAKIMI Ashtakiwa kwa kesi ya Ubakaji nchini Ufaransa

-rickmedia: Rick

Rick

1 week ago
rickmedia: hakimi-ashtakiwa-kwa-kesi-ubakaji-nchini-ufaransa-694-rickmedia

Beki wa klabu ya Paris St-Germain na nahodha wa timu ya taifa ya Morocco, Achraf Hakimi, amethibitisha kuwa anajiandaa kukabiliana na kesi ya ubakaji inayomkabili nchini Ufaransa.

Hatua hiyo inakuja kufuatia madai yaliyotolewa na mwanamke mmoja anayemtuhumu nyota huyo kwa kumfanyia ukatili huo wa kijinsia nyumbani kwake jijini Paris mwaka 2023. Wakati huo, mlalamikaji alikuwa na umri wa miaka 24. Hakimi amekuwa akikana vikali tuhuma hizo tangu zilipoanza kufanyiwa uchunguzi wa awali na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Nanterre mnamo Machi 2023.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Hakimi alielezea kutoridhishwa kwake na mfumo huo lakini akasisitiza utayari wake kusafisha jina lake:

"Leo hii, tuhuma za ubakaji zinatosha kuhalalisha kufanyika kwa kesi. Nasubiri kesi hii ianze kusikilizwa, ambayo itaruhusu ukweli kujulikana hadharani."


Wakili wa mchezaji huyo amethibitisha kuwa "kesi imeshaamuriwa" na kwamba mteja wake ana azma ya dhati ya kuona haki ikitendeka. Hadi sasa, tarehe rasmi ya kuanza kwa shauri hilo bado haijapangwa.